MSEMAJI MKUU WA SERIKALI ATEMBELEA OFISI ZA TANAPA MAKAO MAKUU - ARUSHA

Posted On: Mar, 06 2024
News Images

Mkurugenzi wa idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Mobhare Matinyi leo tarehe 05.03.2024 ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na kukutana na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Mussa Juma Kuji, na kisha kufanya kikao kifupi na Menejimenti ya TANAPA jijini, Arusha

Bw. Mobhare Matinyi atafanya Ziara ya siku 3 kutembelea Hifadhi za Taifa na kujionea shughuli za Utalii na Uhifadhi na kukagua miundombinu hasa barabara katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.