BODI YA WADHAMINI TANAPA YAZINDUA OFISI MPYA YA TANAPA KANDA YA KUSINI

Posted On: Apr, 30 2024
News Images

Bodi ya wadhamini Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inayoongozwa na Mwenyekiti, Jenerali (Mstaafu) George Waitara , ilizindua Ofisi mpya ya Makao Makuu ya Kanda ya Kusini - TANAPA yaliyopo wilayani Mbarali Mkoani Mbeya tarehe 28.04.2024.

Sherehe hizo za uzinduzi Jenerali Waitara aliambatana na Wajumbe wa Bodi ya TANAPA, Mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Samwel Swedi, Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA na viongozi wengine Waandamizi wa Chama na Serikali.

Jengo hilo lina jumla ya Ofisi 19, Ukumbi mmoja wa kisasa wa Mikutano wenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 100 na Maktaba moja.

Ofisi hiyo imegharimu jumla ya kiasi cha shilingi millioni 891.