News

RAIS SAMIA ATOA FIDIA BILLIONI 59 KWA WAKAZI WA NYATWALI WILAYANI BUNDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa kiasi cha Tshs. Billioni 59 kwa ajili ya zoezi la ulipaji fidia kwa wakazi wa kata ya Nyatwali iliyopo Wilayani Bunda, Mkoani Mara. Zoezi hilo la ulipaji fidia limeongozwa na Mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe.Dkt. Vicent Anney ambapo jumla ya wakazi 4111 wa kata ya Nyatwali leo wameanza kulipwa fidia ili kupisha eneo la ushoroba wa Hifadhi ya Taifa Serengeti kwa ajili ya Uhifadhi na uendelezaji wa eneo hilo ambalo ni mapitio ya Wanyama hasa Tembo huku ikitaarifiwa kuwa eneo hatarishi kwa Maisha ya wananchi hao. Read More

Posted On: Sep 10, 2024

ZAIDI YA WATANZANIA 500 KUSHEREHEKEA SIKU YA UHURU KATIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana na makampuni ya waongoza watalii nchini imepanga kuwapeleka watanzania zaidi ya 500 katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kusherehekea siku ya uhuru kupitia kampeni ya “Twenzetu Kileleni 2024” ikiwa ni msimu wa Nne wa Kampeni hiyo yenye Kaulimbiu isemayo “Stawisha Uoto wa Asili Tanzania, Okoa Barafu ya Mlima Kilimanjaro” kampeni ambayo imezunduliwa leo Septemba 6, 2024 hadi Disemba 4, 2024. Read More

Posted On: Sep 07, 2024

MIAKA 60 YA HIFADHI YA TAIFA MIKUMI YAZAA MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA UTALII

Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa Mikumi imeleta mafanikio makubwa katika Sekta ya Utalii nchini yakichangiwa na jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Read More

Posted On: Sep 01, 2024

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aipongeza TANAPA ushiriki wa tamasha la Kizimkazi- Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan amekabidhi cheti cha pongezi kwa ushiriki wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwenye tamasha la Kizimkazi Festival 2024 Hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo Kizimkazi Zanzibar. Cheti hicho cha pongezi kimepokelewa kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Nassoro Juma Kuji, na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Jully Bede Lyimo - Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara pamoja na Afisa Uhifadhi Mwandamizi Amina R. Salum ambaye ni Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa Ruaha. TANAPA, kwa dhati na unyenyekevu mkubwa tumepokea na kuthamini heshima hii kubwa kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan. Read More

Posted On: Aug 25, 2024

MABULA: TANAPA SHIRIKIANENI NA TTB KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NDANI NA NJE YA NCHI.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Utalii - Nkoba Mabula alitembelea Hifadhi ya Taifa Arusha na kujionea vivutio vya Utalii vinavyopatikana vinavyopatina hifadhini, ziara hiyo aliifanya Julai 16.07.2024 jijini Arusha. Read More

Posted On: Jul 17, 2024

RAMADHANI BROTHERS WALITEMBELEA HIFADHI YA TAIFA - SERENGETI

​Washindi wa tuzo za American Got Talent, ambao ni wasanii katika mchezo wa sarakasi, Ramadhani Brothers walifikisha tuzo hiyo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti tarehe 07.04.2024 baada ya kuifikisha katika kilele cha Mlima Kilimanjaro tarehe 03.04.2024 Read More

Posted On: May 11, 2024