HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

                                                                                          tnplogo   

KUHUDHURIA USAILI WA AWAMU YA PILI KWA NAFASI YA UASKARI KATIKA SHIRIKA

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) lilitangaza nafasi za kazi kwa kada ya Askari kuanzia tarehe 03-23/04/2017 na baadae kufanyika usaili wa awali katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Oljoro kuanzia tarehe 22/05/2017 hadi tarehe 25/05/2017.

Baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya usaili kwa nafasi tajwa hapo juu, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania linapenda kuwataarifu waombaji wafuatao hapo chini kuwa wamefaulu kuingia awamu ya pili ya usaili utakaohusisha mafunzo kwa vitendo kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu katika kituo cha mafunzo cha Shirika cha Mlele kilichopo katika Hifadhi ya Taifa Katavi.

Waombaji wote walioitwa wanatakiwa kufika katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi saa nne asubuhi siku ya Jumapili tarehe 20/08/2017 tayari kwa safari ya kwenda Mlele. Inashauriwa waombaji hao kuwepo katika Mji wa Mpanda tarehe 19/08/2017 ili kuepusha usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

NB:Kila mhusika anatakiwa kuwasilisha nakala halisi ya cheti (Original

           Certificate) cha kidato cha nne.  

 

  pdf  Majina ya walioitwa kwenye usaili wa pili