OFA MAALUM KWA WATALII WA NDANI KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA

Katika kuhamasisha utalii wa ndani, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linapenda kuwajulisha kuwa, kutakuwa na safari za kwenda kutalii katika hifadhi za Taifa Ruaha, Tarangire na Serengeti kama ifuatavyo.
a) Utalii wa kwenda Serengeti: Nane nane Kitaifa Simiyu -Mjini Bariadi
Serengeti ni hifadhi maarufu duniani kwa kuwa na msururu wa wanyama wengi wanaohama kutoka eneo moja la hifadhi kwenda jingine. Hifadhi hii ina sifa nyingi sana
ikiwemo uwanda mpana sana wa nyasi, uwepo wa wanyama maarufu watano (the big 5) yaani Simba, Tembo, Faru, Chui na Nyati. Tukibahatika siku hiyo tunaweza kuwaona wote.
Tunayofuraha kuwapeleka Watanzania kutembelea hifadhi hii maarufu katika msimu huu wa Nane Nane kwa bei nafuu kabisa kutokea Mkoani Simiyu.
Kutoka Simiyu kutakuwa na mabasi mawili (2) aina ya Coaster yenye uwezo wa kubeba watalii 28 kila moja kwenda Serengeti na kurudi Bariadi (day trip). Safari hizi zitafanyika tarehe 8/8/2018 tu.
Ili kupata muda mzuri wa kutalii, magari yataondoka saa 12.00 asubuhi na kurudi mjini Bariadi saa 1 jioni siku hiyo.
Tutafanya utalii maeneo mengi ya hifadhi hadi Seronera-eneo ambalo lipo katikati ya hifadhi na lenye maeneo mengi ya kuona wanyama wengi zaidi kwa wakati mmoja. Huduma ya chakula tutapata hapa Seronera, ambapo bei ya chakula ni kuanzia Tsh 6000.
Gharama ya safari nzima itakuwa Tsh 30,000 watu wazima na Tsh 15,000 watoto.
Gharama hii inajumuisha usafiri wa kwenda na kurudi,mwongoza watalii na kiingilio. Ewe Mtanzania, hii si ya kuikosa kwani ni kwa mara ya kwanza kabisa ofa hii kutokea, usisubiri kusimuliwa jipange, jiandae, njoo jiandikishe kwenye banda letu lililopo kwenye viwanja vya maonesho ya nane nane kuanzia tarehe 1.8.2018 hadi tarehe 7.8.2018. Wahi nafasi ni chache.
Jiachie na Jifunze Kitalii.
b) Utalii wa Kwenda Ruaha na Tarangire: Nanenane Jijini Dodoma
Kwa mara ya kwanza tangu Dodoma itangazwe kuwa Jiji, TANAPA inawaletea Watanzania Safari za kwenda kutalii katika hifadhi za Taifa Ruaha na Tarangire kutokea jijini Dodoma.
Safari hizi ni za kwenda na kulala hifadhini. Huduma za malazi zitakuwa katika nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na shirika (Bandas).
Kutokea Dodoma kutakuwa na tripu mbili (2) za kwenda Tarangire na tripu mbili (2) kwenda Ruaha kwa kutumia mabasi aina ya Coaster yenye uwezo wa kubeba watu 26.
Hifadhi za Taifa Ruaha na Tarangire ni maarufu kwa kuwa na makundi makubwa ya Tembo na miti mikubwa aina ya miombo. Pia hifadhi hizi zote zina mto unaopita katikati yake, yaani mto Ruaha kwa hifadhi ya Taifa Ruaha na Mto Tarangire kwa Hifadhi ya Taifa Tarangire. Majina ya mito hii ndio haswaa majina ya Hifadhi hizi.
Japokuwa Ruaha ndio hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania, Tarangire inapendeza kwa kuwa na uwanda mpana unaokuwezesha kuona vivutio vingi.
Gharama: Gharama itakuwa Tsh 60,000 kwa mtu mzima Tsh 40,000 kwa mtoto.
Gharama hii inajumuisha usafiri kwenda na kurudi (Dodoma-Ruaha-Dodoma)-Dodoma- Tarangire-Dodoma, kiingilio, mwongoza watalii na Malazi hifadhini.
Kwa kuwa hizi ni safari za kulala, ni vyema watoto waambatane na wazazi wao.
Siku za kwenda kutalii: Safari ya kwanza tarehe 4.08.2018 kurudi tarehe 5.08.2018 : Safari ya pili tarehe 8.08.2018 kurudi tarehe 9.08.2018
Zingatia:
1. Mtoto anayelipa ni mwenye umri kati ya miaka 5 hadi 16. Zaidi ya miaka 16 analipa kama mtu mzima.
2. Gharama za matumizi binafsi ni juu yako, bei ya chakula inaanzia Tsh 6000 hadi Tsh 12,000.
3. Gharama hizi ni pamoja na VAT (18%)
4. Malipo yanapokelewa kwa njia ya kadi za Visa, Masta na Tembo. Ili kulipia na
kujiandikisha fika katika banda la TANAPA viwanja vya nane nane. Banda hili lipo
katika banda kuu la Wizara ya Maliasili na Utalii.
5. Mwisho wa ofa hii ni tarehe 8.8.2018
6. Ofa hii ni kwa raia wa Tanzania tu


Mawasiliano:
Tupigie simu: Kwa maelezo ya jumla na safari za Ruaha na Tarangire 0742272318 Kwa safari za Serengeti 0783464974
Barua pepe: marketing@tanzaniaparks.go.tz
Jiachie na Jifunze Kitalii