HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba matangazo ya ajira yanayosambaa katika vyombo mbalimbali vya mawasiliano SI SAHIHI na kwamba TANAPA haijatangaza nafasi zozote za kazi kama inavyosambazwa.

Aidha, Shirika linaufahamisha umma kuwa mara baada ya kuainisha nafasi mbalimbali za ajira zinazotakiwa kujazwa, matangazo hutolewa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama magazeti na tovuti ya Shirika.  Maombi ya nafasi za kazi hutumwa kwa njia ya mtandao “Aruti recruitment Portal” na SI VINGINEVYO.

Hivyo, tunapenda kutoa angalizo kwamba utaratibu wowote wa matangazo ya ajira kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania utakaoenda kinyume na huu, tafadhali upuuze.

Imetolewa na
Kamishna wa Uhifadhi
Hifadhi za Taifa Tanzania
S. L. P 3134
ARUSHA.

Barua pepe:  info@tanzaniaparks.go.tz
dg@tanzaniaparks.go.tz

Simu:  +255 (27) 297 0404-07