TAARIFA KWA UMMA

KUJIUNGA RASMI KWENYE MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO WA SERIKALI (GePG)

Sheria ya Fedha za Umma Sura Na. 348 ya mwaka 2017 inataka mashirika na taasisi za serikali kukusanya mapato kupitia mfumo wa GePG.

Ikumbukwe kwamba TANAPA imekuwa ikipokea malipo ya kuingia hifadhini kupitia mtandao (Online Reservation and Payment System) na kufuatia sheria hii TANAPA imefanya mabadiliko madogo katika mfumo kuwezesha namba ya malipo (Payment Control No.) kutoka GePG kutumika badala ya order namba.

Majaribio yataanza rasmi kwa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro tarehe 14 Septemba 2018 kwa kipindi cha siku 7. Hifadhi nyingine zitafuata baada ya hifadhi hii kuonesha mafanikio.

Kwa msaada na maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia anuani ifuatayo:-

Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu

Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),

Mwalim Nyerere Conservation Center,

Burka Estate – Dodoma Road

S.L.P 3134,

Simu: +255 27 2970404-5

ARUSHA TANZANIA.

Email: ict@tanzaniaparks.go.tz

Imetolewa na: Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Tanzania National Parks.